Maamuzi Mazito Basata, Rayvanny Kuirudisha YouTube ‘NYEGEZI MWANZA’

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limetoa kauli kuhusiana na video ya Mwanza ya Rayvanny akimshirikisha Diamond Platnumz baada ya video hiyo kurudishwa katika mtandao wa YouTube na Rayvanny June 15.
Basata wamekanusha taarifa zinazoenea katika mitandao kwamba video hiyo imeruhusiwa huku akimtaka Rayvanny na Uongozi wake kuifuta video hiyo haraka katika mtandao wa YouTube.
 
 
Kwa upande wa Meneja wa Label ya Wasafi, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ ameliambia gazeti la Risasi kwamba;
“Sisi hatupo tayari kukwaruzana na Basata katika hilo, kama nilivyosema awali tutahakikisha tunatekeleza maagizo yao yote, haya yanayotokea ya video kurudi yapo nje ya uwezo wetu katika maswala ya kiufundi zaidi kwani kila tukiitoa kuna mtu anairudisha, tumeshaanza kuwasiliana na mamlaka za masuala ya mitandao kulishughulikia hilo,” alimaliza Babu Tale.
- ISIKUPITE:RAYVANNY AFUNGUKA KUHUSIANA NA MWANZA NYEGEZI
 
			

Comments are closed.