×

Mabasi Mwendo Kasi Yagongana, Yasababisha Foleni Shekilango

mabasi ya mwendo kasi
Wananchi wakiwa kituo cha mabasi ya mwendo kasi wakisubiri kukata tiketi za mabasi ya mwendo kasi kituo cha Shekilango, Barabara ya Morogoro.
mabasi ya mwendo kasi
Mabaki ya vioo vilivyovunjika baada ya mabasi hayo kugongana.

mabasi ya mwendo kasi

ASUBUHI ya leo katika eneo la makutano ya barabara za Morogoro Shekilango jijini Dar es Salaam, palikuwa na foleni ndefu kutokana na mabasi ya mwendo kasi kugongana eneo hilo.

Basi lilivyoharibiwa kwa mbele.
Basi lilivyoharibiwa kwa nyumba.

Mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wamesema ajali hiyo ilitokana na basi moja la mwendo kasi kuligonga kwa nyuma basi jingine eneo la mataa ya Shekilango wakati linatoka Manzese, jambo lililosababisha foleni ndefu kabla ya magari hayo kuondolewa eneo hilo.

Hata hivyo, katika ajali hiyo, hakuna mtu yeyote aliyepoteza maisha au kujeruhiwa. Mtandao huu ulijaribu kuwasiliana na jeshi la polisi lakini haukupata mtu wa kulizungumzia suala hilo.

Mabasi ya Mwendokasi Yagongana, Yasababisha Kizaazaa Shekilango- Dar

Leave a Comment