The House of Favourite Newspapers

Madaha: Plizi Msinifananishe na Amber Rutty

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva ambaye pia ni msanii wa filamu, Baby Madaha ameibuka na kueleza kwamba muziki wake siyo wa kiki bali anafanya muziki wa kweli hivyo asifananishwe na Amber Rutty.

 

Akistorisha na Amani, Baby Madaha alisema kwa sasa amekua hawezi kufanya kiki za kijinga kama Amber Rutty kwani zitamshushia hadhi hivyo amekuwa akifanya jitihada ili akubalike kwa kazi nzuri na siyo kwa kiki tena kama zamani.

 

“Wasanii wanaofanya kiki hasa wakiwa na ngoma mpya hao ni wafanyabiashara lakini mimi ni mwanamuziki ndiyo maana nimetoa ngoma mpya hata sijafanya kiki maana zina madhara mengi kwani kuna mastaa wakubwa wamekuwa wakiteswa sana na kiki na zimekuwa kikwazo kikubwa kwao,” alisema Baby Madaha anayetamba na Ngoma ya Mjanja Wangu.

Stori: Gladness Mallya

Comments are closed.