Maduro Afikishwa Mahakama baada ya Kukamatwa na Marekani

Rais wa zamani wa Venezuela aliyeondolewa madarakani, Nicolás Maduro, amefikishwa katika Mahakama ya Shirikisho ya Manhattan leo Januari 5, 2026 kujibu mashtaka yanayomkabili.
Maduro anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi unaohusishwa na biashara ya dawa za kulevya (narco-terrorism), siku chache baada ya kukamatwa kwake na jeshi la Marekani tukio lililozua sintofahamu kubwa kuhusu mustakabali wa taifa hilo lenye utajiri wa mafuta barani Amerika Kusini.
Maduro na mke wake, Cilia Flores, wamewekwa kizuizini katika Gereza la Brooklyn baada ya vikosi vya Marekani kuwakamata mjini Caracas katika oparesheni ya kushtukiza iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Kesi hiyo inatarajiwa kuvutia hisia za kimataifa huku maswali yakiongezeka kuhusu mwelekeo wa kisiasa na kiusalama wa Venezuela.

