×

Maelfu Wajitokeza Kuuaga Mwili wa Malkia Elizabeth katika Ukumbi wa Westminster London

Maelfu ya waombolezaji kutoka matabaka mbalimbali wamejitokeza kuuaga mwili wa Malkia Elizabeth katika ukumbi wa jadi wa Westminster mjini London.

 

Jeneza la Malkia huyo aliyeongoza kwa miongo saba litakaa hapo ukumbini kwa siku nne kabla ya mazishi yake Jumatatu wiki ijayo.

Baada ya siku kadhaa za kupitishwa katika maeneo mbalimbali na kufanywa taratibu za Kifalme wakati mwili wa malkia huyo ukiletwa mjini London kutoka kasri ya Balmoral nchini Scotland, ambako alifariki dunia Alhamisi iliyopita akiwa na umri wa miaka 96, hii ilikuwa fursa ya watu wa kawaida kushiriki moja kwa moja katika hafla hiyo.

 

Maafisa wanatarajia kuwa karibu watu 750,000 watajitokeza kutizama jeneza la Malkia huyo kabla ya Jumatatu asubuhi.

 

Mazishi ya malkia yamepangwa kufanyika Septemba 19, 2022 huko Westminster Abbey. Jeneza hilo baadae litachukuliwa kwenda Windsor kwa ajili ya ibada ya mazishi, ambapo mume wa malkia, Prince Philip, ndipo alipozikwa mwezi Aprili 2021.

Leave a Comment