The House of Favourite Newspapers

JPM AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI BARABARA YA KIMARA – KIBAHA (Video +Picha)

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata Utepe na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Kisiasa pamoja na Viongozi wa Dini wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.

Rais Dkt. John Magufuli ameeleza kushangazwa kwake na kitendo cha Mbunge wa Kibamba (CHADEMA), John Mnyika kwa kutokuwa muungwana, akitaka angalau aipongeze Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kumpelekea maji jimboni kwake.

 

Magufuli amesema hayo leo wakati wa ujenzi wa Barabara ya Morogoro kwa njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha leo, Jumatano, Desemba 19, 2018 maeneo ya Kimara Stop Over.

 

“Nilitegemea atakaposimama hapa angesema asanteni sana CCM, demokrasia ya namna gani anaitaka, hata kufunika midomo usiongee nayo ni demokrasia. Demokrasia siyo fujo, watu wafanye fujo mitaani wabomoe maduka halafu tuwaache eti kisa ni demokrasia? Haiwezekani. Demokaria ya kweli imehamia bungeni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Kisiasa pamoja na Viongozi wa Dini kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.

“Napenda kuwaambia ndugu zangu wa eneo hili la Kimara kuwa, ukivamia sehemu ya barabara ujue kabisa umetafuta umaskini, hivyo anayewaambia kua kuna fidia, mimi ninawaambia fidia haipo, narudia tena fidia haipo, fidia haipo.

 

Awali Mnyika alimuomba Rais Magufuli kuwalipa fidia wananchi waliyobomolewa nyumba zao katika eneo la Kimara kupisha upanuzi wa barabara hiyo, lakini Rais amesisitiza kuwa serikali haitalipa fidia kwa watu waliyobomolewa nyumba zao kwa kuwa walikuwa wamejenga ndani ya hifadhi ya barabara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai mara baada ya kufunua kitambaa kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.

“Wapo wanasema vyuma vimekaza, vitakaza kweli, asiyefanya kazi na asile, lazima tuwaambie ukweli hii ya vyuma vimekaza ni watu wanazushazusha. Wananchi wa Ubungo muache kulalamika vyuma vimekaza, mkatafute kazi ya hata ya kuchimba mtaro hivyo vyuma mtavibanua.

“Ninawaomba Watanzania wote, hebu tujiamni basi angalau kwa miaka mitano, nikishaondoka muache kujiamini, mfanye mnavyotaka. Kwa nchi inayojitambua hatuwezi kusubiri misaada, mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe, nchi hii sio katili. Tuheshimu Sheria zetu, nafahamu Sheria ni ngumu na ndiyo maana unakuta hata sheria za Mussa hatuziheshimu, usitamani mwanamke wa mtu unakuta kila mtu anatamani tu.

“Kuna watu wanasema eti ni kodi zetu, kwani zamani mlikuwa hamlipi kodi? Mmbona hazikujengwa? Kwa nini msiseme tu kuwa ni juhudi za Rais Magufuli? Watu wamefariki kwa kushindwa kuwahi Muhimbili kwa ajili ya msongamano wa barabara hii, ndoa zimevunjika mtu anatumia sababu ya msongamano anarudi nyumbani usiku kumbe alikuwa pembeni anasema msongamano kumbe jamaa analiwa,” amesema Magufuli.

VIDEO: MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA

Comments are closed.