Makazi Mapya Waliohamishwa Ngorongoro Yanoga
Wawakilishi wa wananchi walioamua kuondoka kwa hiari kutoka kata 10 kati ya kata 11 ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwenda Msomera Wilayani Handeni mkoani Tanga jana Aprili 10 mwaka huu wamefika eneo hilo la Msomera na kujionea hali halisi.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kushuhudia mradi huo wa awamu ya kwanza wenye jumla ya kaya 35 waliweza kushuhudia moja ya kisima kati ya visima tano kilichopo maeneo ya biashara tayari kwa kuzalisha maji zaidi ya lita 2000 mpaka 3000 kwa saa moja. Mpaka sasa ujenzi huo umeshamilika kwa asilimia 60 na sehamu nyingine ya visima itakuwepo ambapo vinaendelea kuchimbwa.
Visima hivyo ni pamoja na eneo la malisho ya mifugo na sehemu za majosho ambapo josho lingine lipo Kijiji cha Msomera ambapo maeneo ya makazi nayo yapo tayari kwaajili ya wananchi kuanza kuhamia.
Wakiwa Msovero Wilayani Handeni mkoa wa Tanga, baadhi ya wawakilishi hao kwa pamoja baada ya kuona makazi hayo mapya eneo hilo watakalohamishiwa wamejionea kwa macho yao huduma za msingi ikiwemo afya ambapo walikutana pia na mganga mfawidhi wa zahanati ya kijiji pia katika elimu walikutana na mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Msovero sehemu zote hizo walikaribiswa vizuri, na kuoneshwa miundombinu inaendelea kuboreshwa ili wasisite kuhamia.
Wawakilishi hao wa wenzao wameomba mchakato huo uharakishwe ili kuwa mfano kwa wengine wanaosita kuhama Ngorongoro kwani eneo hilo licha ya wao kukubali kwa hiari kuhama kwenda Handeni bado wanakumbana na vitisho kwa wasio tayari kuondoka.
Maendeleo ni kitu kimojawapo kinachotazamiwa na kila mwanadamu lakini kwa wakazi wa Ngorongoro imekuwa ni ndoto kutimiza moja kwa moja matamanio yao kwa sababu eneo hilo la uhifadhi ni eneo ambalo hutunzwa hivyo vitu vyenye uashiria wa uharibifu wa hifadhi hupigwa marufuku mfano, ujenzi wa nyumba za tofali, hivyo wakazi hawa hulazimika kuishi kwenye nyumba za nyasi na udongo hivyo kuwacheleweshea wakazi, lakini wakiwa eneo la Msovero maendeleo yanajidhihirisha kwani wamepewa uwezo wa kujenga na kumiliki ardhi na kujiendeleza na shughuli zote za halali za kujipatia kipato.
Ongezeko la wanyama pori waharibifu mfano tembo pia limekuwa ni sababu ya wakazi hawa kufanya maamuzi ya kuhama kwa hiyari kwani wanyama hao wamekuwa wakifika hadi kwenye makazi yao hali ambayo unapelekea pia usalama wa maisha yao kuwa mdogo lakini eneo hili watakalohamia hali ni shwari hakuna kiashiria vya wanyama wakali wala waharibifu hivyo usalama wao unatazamiwa kuwa mzuri.
Changamoto nyingine ni umbali uliopo kati ya wakazi na huduma za kijamii mfano hospitali, shule nakadhalika uhitaji wa haraka wa huduma za dharura mfano mjamzito au mgonjwa kuwahishwa hospitali imekuwa hiyo kati ya sababu inayopelekea wakazi hawa kufanya maamuzi ya kuhama kwa hiyari kwani umbali wa huduma hizi unapelekea madhara makubwa mathalani vifo pindi wakazi hawa wanapohitaji huduma hizo, hili pia limepatiwa majibu katika Kijiji cha Msovero kwani huduma hizo za kijamii zipo katika makazi hayo mapya.
Kukosekana kwa usafiri mdogo almarufu kama bodaboda katika muktadha wa ajira katika wilaya ya Ngorongoro pia imekuwa ni ushawishi mkubwa kwa vijana waishio eneo hili la uhifadhi kufanya maamuzi ya kuhama kwa hiyari kwani ni kwa kipindi kirefu vijana wakiwa wanatafuta ajira za kujikwamua ki uchumi lakini shughuli hizo hazina nafasi hifadhini kwa furaha wameweza kuiona fursa hiyo iliyopo katika makazi mapya, walisema wananchi hao waliowawakilisha wenzao kukagua makazi hayo mapya.