The House of Favourite Newspapers

 Malaika aelezea ukimya wake

BAADA ya kuwa kimya kwa muda mrefu, mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Diana Exavery ‘Malaika’ ameeleza ukimya wake umesababishwa na kujipanga lakini pia kukwepa ‘vita’ na binadamu.  Malaika aliiambia Risasi Vibes kuwa, ameamua kukaa na kutafakari mambo mengi yaliopita kwenye maisha yake na ndiyo maana amekuwa kimya na ahitaji kufanya vita na mtu yeyote zaidi ya Mungu tu.

“Unajua nipo kimya kwa sababu napanga mambo yangu mengi na kingine sihitaji vita na binadamu ukiwa kimya hiyo inasaidia usikumbane na mambo ya ajabu, sasa hivi namtumainia aliye juu tu na si kingine,” alisema Malaika

Comments are closed.