The House of Favourite Newspapers

Mama Dangote Kumfukuza Anko Shamte

0

WIKI kadhaa baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa, staa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemfukuza baba yake mlezi nyumbani kwa mama yake, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’, Maisara Shamte almaarufu Uncle Shamte, mama huyo amefyatuka kila kitu kinachoendelea, IJUMAA lina stori maalum (exclusive).

 

MADAI YA MONDI KUMFUKUZA UNCLE SHAMTE

Kabla ya kumsikia Mama Dangote alichosema, awali kulisambaa habari hizo nzito na za kushtua zilizodai kwamba; Diamond au Mondi anachukukizwa mno na uwepo wa Uncle Shamte nyumbani kwa Mama Dangote, Madale jijini Dar, akila, kunywa na kulala bure.

 

Ilidaiwa kwamba, ugomvi huo ulikuwa mkubwa baada ya Mama Dangote kusimama upande wa Uncle Shamte akidai kwamba hataki mwanaume wake huyo aguswe na wala asiambiwe kitu na mtu yeyote na kwamba nyumbani hapo kwake.

 

Ugomvi huo unatajwa kuwa mkubwa kwa sababu, kwa mara ya kwanza, Mama Dangote anadaiwa kutofautiana waziwazi na Mondi ambaye alisema hataki kumuona jamaa huyo nyumbani hapo, jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa kwenye maisha yao kwani huwa jambo la mmoja ni la wao wawili kutokana na ‘bondi’ waliyonayo.

 

EXCLUSIVE NA MAMA DANGOTE

Katikati ya mambo mengi yanayozungumzwa, Gazeti la IJUMAA limefanya mahojiano maalum (exclusive interview) na Mama Dangote ambaye anafunguka kuhusiana na madai hayo mazito dhidi ya mwanawe na Uncle Shamte.

 

Kwanza, Mama Dangote anasema kwamba, Uncle Shamte ni mumewe halali ambapo hakuna kitu kama hicho.

Mama Dangote anasema kuwa, hana sababu ya kujieleza sana kwa sababu ukweli wote wa kile kinachoendelea wanaujua wao.

 

Mama huyo mzaa-chema anasema kuwa, anawashangaa mno baadhi ya watu kuzusha jambo kama hilo, lakini yeye haoni kitu cha ajabu kwa sababu watu wengi wanapenda kuishi katika maisha ya kimtandaoni siku zote hivyo kazi yao ni kumchungulia ameposti nini na nani amefanya nini, ndiyo mambo yaliyopo kwa baadhi ya watu.

 

“Naona labda ni kwa sababu siku hizi simposti sana (Uncle Shamte) na hiyo imetokea kwa sababu kuna kipindi unaamua kuyaweka maisha yako kuwa binafsi zaidi, lakini watu wakiona hivyo wanajua kuwa tayari mmegombana, kumbe siyo.

“Kuna wakati watu wanapenda kuishi maisha yao peke yao bila watu wengine kujua kinachoendelea,” anasema Mama Dangote.

 

Akiendelea kuzungumza na Gazeti la IJUMAA, Mama Dangote anasema kuwa, watu walivyoona Uncle Shamte ameposti kwenye ukurasa wake wa kijamii kuwa amekosa kuhudhuria birthday ya mtoto wake (Diamond) kwa sababu amefukuzwa (ndivyo Uncle Shamte alivyomwambia Rommy Jons) ndipo ukazuka mjadala huo wa wao kuachana.

 

Mama Dangote anasema kuwa, hilo ndilo tatizo la mitandao ya kijamii kwa sababu wakati mwingine unakuta mtu anataniana na mtu wake, lakini wengine wanaamini kila kitu wanachokiona mtandaoni.

“Shida ya watu wengi wanaamini kila kitu wanachokiona kwenye mitandao ya kijamii, kitu ambacho siyo sahihi kabisa na wasione kila wakionacho ndicho hicho.

 

“Mimi ninawaambia tu watu kwamba wakumbuke kuna wakati watu wanataka kuishi maisha yao wenyewe bila mtu kujua chochote kutoka kwao na ndiyo maisha mazuri,” anasema Mama Dangote.

 

IJUMAA NA UNCLE SHAMTE

Na katika kuthibitisha kwamba hawana tatizo lolote, Mama Dangote alimuunganisha Mwandishi wa Gazeti la IJUMAA na Uncle Shamte na kuzungumza naye kuhusiana na sakata hilo;

IJUMAA: Uncle Shamte habari yako?

 

UNCLE SHAMTE: Salama kabisa, niambe, kuna habari gani kutoka IJUMAA?

IJUMAA: Kuna tetesi kuwa umeachana na Mama Dangote, lakini sasa naona wazi mko pamoja na sina lingine jipya…

 

UNCLE SHAMTE: Basi nashukuru sana kama na wewe mwenyewe umeamini tuko pamoja kwa sababu naona watu wanapenda sana itokee hivyo, sisi tuko vizuri kabisa.

IJUMAA: Nashuru sana Uncle Shamte endelea kumtunza Mama Dangote.

UNCLE SHAMTE: Asante sana na karibu tena.

 

MAMA DANGOTE: Haya nafikiri sasa umeelewa vizuri kabisa, hatuna tatizo lolote.

IJUMAA: Nashukuru Mama Dangote kwa kupata ukweli wako.

MAMA DANGOTE: Asante, karibu sana.

 

SI MARA YA KWANZA

Si mara ya kwanza kwa Mama Dangote na Uncle Shamte ambao wamefunga ndoa halali kudai kuachana.

Kuna wakati ilisemekana kwamba walitibuana baada ya Umcle Shamte kudaiwa kuchepuka na kupata mtoto nje ya ndoa, lakini Mama Dangote amefunga mjadala huo kwamba, siyo wa kuachana leo wala kesho hivyo watu wakae kwa kutulia.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply