The House of Favourite Newspapers

Mamia Ya Wakimbiaji Tigo ‘Kili Marathon’ Dar Wafurika Mlimani City Kuchukua Namba Na Vifaa Vya Kukimbilia

0
Picha tofauti zikionesha zoezi hilo lilivyokuwa likiendeshwa leo.

Dar es Salaam 17 Februari 2024: Mamia ya wakimbiaji wa Tigo ‘Kili Marathon’ Km 21, wakazi wa Jiji la Dar, leo wamejitokeza katika Viwanja vya Mlimani City kwa ajili ya kuchukua namba na vifaa vya kukimbilia mbio hiyo inayotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo Februari 25 mwaka huu.

Zoezi hilo linaendelea tena kesho kuanzia saa sita mchana mpaka saa kumi na moja jioni ambapo mmoja wa waratibu wa zoezi hilo aliwasihi watakaokuja kesho kuwahi mapema kabla ya muda wa kusitisha zoezi hilo ifikapo saa kumi na moja kamili za jioni.

Akizungumza baada ya kupata namba na vifaa vya kukimbilia mmoja wa wakimbiaji wa mbio hiyo alisema yeye ni mtumiaji mkubwa wa mtandao wa Tigo na muda wote amekuwa akiinjoi anapotumia mtandao huo ndiyo maana ameamua kukimbia mbio hiyo kwaajili ya kuisapoti Tigo.                                                                                                                         HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS/ GPL

Leave A Reply