Man City yatenga bilioni 500 za usajili

Pep Guardiola

WAKATI kukiwa na furaha kwenye kikosi cha Manchester City kocha wa timu hiyo Pep Guardiola, amesema kuwa anataka kutengeneza kikosi imara.

 

City wana uhakika kuwa msimu ujao watakutana na upinzani mkubwa sana kwenye ligi na hivyo wanatakiwa kuhakikisha wanafanya usajili sahihi.

 

Guardiola amesema anataka kufanya usajili wa wachezaji wapya wenye thamani ya pauni milioni 200 (zaidi ya shilingi
bilioni 500).

Guardiola anataka kuhakikisha anatwaa tena ubingwa wa England msimu ujao na taarifa zinasema
kuwa baada ya msimu ujao kocha huyo anapanga kutimka kwenye ligi hiyo.

 

City wanamwinda kiungo wa Atletico Madrid, Rodri, wakiamini kuwa wanataka mchezaji ambaye anaweza kusaidiana na Fernandinho, ambaye kwa sasa anafikisha miaka 34.

 

Mbali na huyo, City wanamtaka mshambuliaji wa Frankfurt, Luka Jovic, wakati pia wakiwa wana mpango wa kumsajili mchezaji wa Benfica, Joao Felix, 19 ambaye kiwango chake ni cha juu sana msimu huu.

 

Kocha huyo anaamini akiwapata wachezaji hao anaweza kuwa na kikosi imara ambacho kinaweza kuchukua ubingwa tena msimu ujao.


Loading...

Toa comment