Manula atia doa usajili wa Kakolanya Simba

BAADA ya kufanikiwa kuvunja mkataba na Yanga, aliyekuwa kipa namba moja wa timu hiyo, Beno Kakolanya anaweza asijiunge na Simba ambayo inadaiwa kumhitaji.

 

Sababu kubwa ni uhakika wa nafasi ya kucheza kutokana na ushindani wa namba ambao anaweza kukumbana nao kutoka kwa makipa wa sasa wa timu hiyo, Aishi Manula pamoja na Deogratius Munishi‘Dida’.

Aishi Manula

Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja wa Kakolanya, Seleman Haroub, alisema mpaka sasa kipa huyo ana ofa nyingi kutoka kwa timu mbalimbali ila bado hajaamua ni timu gani ataenda kuitumikia kwa sababu anahitaji kumuona anakwenda kucheza na siyo kukaa benchi.

 

Kutokana na hali hiyo, Kakolanya atakuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba kama atajiunga nayo kutokana na ubora wa Manula pamoja na Dida.

 

“Tangu tulipopata barua ya Kakolanya kuachana na Yanga, kuna baadhi ya timu za hapa nchini zimeonyesha nia ya kumtaka ila bado mazungumzo ya kina na timu hizo hayajafanyika. “Lakini nahitaji kumuona anakwenda katika timu ambayo atakuwa na uhakika wa kucheza na siyo kukaa benchi,” alisema Haroub

NIYONZIMA, MUNISH Wafunguka Walipofanya Makosa / Wafurahishwa

Loading...

Toa comment