The House of Favourite Newspapers

Marekani Yatangaza Vikwazo Dhidi ya Viongozi wa Pande Zinazopigana Sudan

0
Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani, Jake Sullivan.

Marekani Alhamisi imetangaza vikwazo dhidi ya viongozi wa Sudan inaowalaumu kwa kukwamisha makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyopatikana chini ya juhudi za Marekani na Saudi Arabia.

Marekani imetangaza vikwazo hivyo baada ya mashambulizi ya makombora na ya anga kuua raia 18 katika soko moja mjini Khartoum ambako mapigano yaliendelea leo Alhamisi baada ya jeshi kujiondoa kwenye mazungumzo ya amani.

Kwa zaidi ya wiki sita, Khartoum na maeneo mengine ya nchi yamekumbwa na vita vya umwagaji damu kati ya jeshi na kikosi cha Rapid Support Forces (RSF), Washington ikisema pande hizo mbili zimehusika kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano na kuchochea umwagaji damu wa kutisha.

“Tunafuatilia hali hiyo kwa kuweka vikwazo na vizuizi vya visa dhidi ya wahusika ambao wanaendeleza ghasia,” mshauri wa masuala ya usalama wa taifa Jake Sullivan amesema katika taarifa.

“Raia 18 waliuawa na 106 kujeruhiwa” kwa shambulio la makombora na mashambulizi ya mabomu na ya anga Jumatano katika soko kusini mwa Khartoum, kamati ya wanasheria wa haki za binadamu imesema.

HALI ILIVYO NDEGE WALIYOPANDA YANGA WAKIELEKEA ALGERIA, UTACHEKA VITUKO vya AFISA HABARI KAMWE

Leave A Reply