The House of Favourite Newspapers

Mashabiki Barca wamtaka Valverde

 MASHABIKI wa Barcelona wanataka Ernesto Valverde abakie kama kocha wa timu hiyo. Valverde anakabiliwa na presha kubwa baada ya Barcelona kutolewa kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
licha ya ukweli kuwa aliisaidia Barcelona kutetea taji lake la La Liga msimu huu wa 2018/19.

 

Barcelona ilikuwa imepania kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini ilikwaa kisiki baada ya kutolewa kimaajabu na Liverpool.

Barcelona ilishinda mchezo wa kwanza mabao 3-0 kwenye uwanja wao wa Nou Camp lakini kinyume cha
matarajio ya wengi ilichapwa mabao 4-0 ugenini na Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield na kutolewa mashindanoni. Hali hiyo haikufurahisha wadau wa Barcelona, ambao baadhi yao walitaka Valverde atimuliwe kutoka katika nafasi hiyo.

 

Valverde, ambaye aliiongoza Barcelona kucheza na Valencia katika fainali ya Copa del Rey hana uhakika wa nafasi yake kwa msimu ujao. Hata hivyo, mashabiki wa Barcelona wanataka Valverde aendelee
kuwa kocha kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na gazeti la Sport la Hispania.

 

“Kwa kweli hata kutolewa kwetu kulichangiwa zaidi na uzembe wa wachezaji na sio kocha Valverde,” alisema shabiki mmoja wakati akichangia maoni yake kwenye gazeti la Sport ambalo lilitaka kujua maoni yao kuhusu mustakabali wa Valverde

Comments are closed.