×

Mashabiki wa Soka Sasa Kufaidi Michuano Kibao Kupitia Startimes Kwa Bei Ileile

Mashabiki wa soka wamesogezewa karibu michuano ya ligi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Carabao Cup, La Liga na michuano mingine ya kimataifa karibu na TV zao kupitia kisimbuzi cha Startimes kwa bei ileile.

Akizungumza na wanahabari leo Julai 31, 2024 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Startimes, David Malisa wakati akizindua kampeni mpya ya Zote Ndani, amesema kampuni hiyo itaendelea kuongeza ubora wa bidhaa kwa wateja wao kuliko kuongeza bei ya vifurushi.

“Msimu huu wa michuano mbalimbali ikiwemo La Liga, EFL Carabao, Roshini Saudi Pro, Copa de Rey na mingine kibao ambayo itakuwa inaoneshwa kupitia Chaneli ya TV3 ndani ya kisimbuzi cha Startimes.”

Malisa ameongeza kuwa kwa takribani miaka 8, Startimes imekuwa ikionesha Michuano ya Bundesliga na kwa msimu ujao wataendelea kuwaletea wateja wao mechi mbalimbali kupitia Startimes kwa lugha ya Kiswahili.

Pia amewasihi Watanzania kununua visimbuzi hivyo ili kushuhudia burudani za Soka, Life Style na tamthilia zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.

Nae Meneja vipindi na Maudhui kutoka TV3, Emmanuel Sikawa amesema michuano hiyo itaruka kupitia TV3 kwa picha angavu yenye ubora zaidi (HD).

Pia amesema Mechi zoe zitaruka kwa Lugha ya Kiswahili kupitia wachambuzi mahili akiwemo Tunu Hassan, Privadinho, Shaffih Dauda na wengine wengi.

“Tumekuwa tukitoa burudani bora kwenye matangazo lakini kwenye hii ‘Zote Ndani’ tutaongeza ubora zaidi na kufanya uchambuzi uliotukuka tukiwa na wachambuzi wabobezi kwenye soka.”

Leave a Comment