The House of Favourite Newspapers

Mastaa kumwangushia Johari pati…

WATU wajipange kukuandalia pati ya kukupongeza kwa kukaa mwezi mmoja bila kunywa pombe; maana yake nini, kama wewe si ‘chapombe’?

Risasi Jumamosi linatafakari hivyo baada ya baadhi ya mastaa wa filamu Bongo kuibuka na kumpongeza msanii mwenzao, Blandina Chagula ‘Johari’ kwa kusitisha kwa muda unywaji wa pombe hadi Mwezi Mtukufu wa Ramadhani upite.

 

Mastaa hao walimwaga pongezi hizo sambamba na ahadi ya kumfanyia pati Johari kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.

“Alipoandika (kwenye ukurasa wake) kuwa hatakunywa pombe hadi Ramadhani iishe mimi nilijua hawezi, lakini anaonekana ataweza, binafsi nampongeza,” aliandika Wema Sepetu.

 

Baada ya pongezi kumimika kwa Johari ndipo mastaa hao walisema pongezi hizo zisiishie hewani bali ziambatane na pati ambayo wamepanga kumfanyia baada ya mfungo kuisha, mwezi ujao.

Yote haya yanatokea kutokana na Johari kudaiwa kuwa ni mtumiaji mzuri wa vilevi anayetajwa kuwa jogoo hawezi kuwika bila mwigizaji huyo kubusti akili kwa pombe.

 

Kutokana na fikra hizo na uwezo aliouonesha wa kupitisha siku takriban 17 (mpaka stori hii inatayarishwa) bila kunywa na kupania kumaliza mwezi mzima ndiko kulikowashangaza wenzake na kuona kumbe hata akiamua kuacha kabisa pombe anaweza.

 

Mastaa waliompa tano Johari ni Wema, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Mayasa Mrisho ‘Maya’, Aunt Ezekiel, Husna Maulid, Husna Idd ‘Sajenti’ na Halima Yahaya ‘Davina’.

STORI: Imelda Mtema, Risasi Jumamosi

Comments are closed.