The House of Favourite Newspapers

MASTAA WAPEWA KIBANO NA TRA

0
Rais Magufuli.

 

IMEFICHUKA! Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeweka wazi kuwa kwa sasa inakula sahani moja na kuwapa kibano kikali mastaa wote wanaokwepa kodi kupitia kazi zao kiasi cha kulikosesha taifa mapato yake yanayostahili, Ijumaa lina full data.

 

Kajala Masanja.

 

TRA HAWA HAPA!

Meneja Msaidizi wa Madeni wa TRA, Mkoa wa Kodi wa Kinondoni, Sylver Rutagwelera aliliambia Ijumaa kuwa, baadhi ya mastaa wamekuwa wagumu kuanika ukweli juu ya makampuni yao na mikataba midogo na mikubwa ya kikazi wanayosainisha, jambo ambalo linaonesha wazi ni ukwepaji wa kodi. “Kila msanii anatakiwa kuchangia anachopaswa kwenye pato la taifa kupitia kazi yake.

Jokate Mwegelo Kidoti.

 

Tunafahamu wapo wasanii na wanamuziki mbalimbali wanaomiliki makampuni lakini wamekuwa wagumu kuyaanika sambamba na kuanika mikataba yao wazi. “Lakini niseme tu TRA ipo macho na itaendelea kula sahani moja nao maana tayari baadhi yao tumekwisha anza nao pamoja na kuwapiga faini juu ya malimbikizo ya madeni  ikiwa ni sambamba na kuwafungia makampuni yao,” alisema Sylver.

 

SIRI YA MADENI YAO YAANIKWA

Sylver alianika baadhi ya mastaa ambao walipigwa faini na kufungiwa makampuni yao lakini baada ya kuanza kulipa waliwafungulia. “Tulikuwa na Rita (Madam) wa Kampuni ya Benchmark Production ambaye alikuwa akidaiwa mamilioni kutoka kwenye kampuni yake ya kwanza (Benchmark Entertainment) lakini baada ya kumfungia alikuja tukakaa naye na kuanza kulipa na sasa tumemfungulia baada ya kuridhishwa na maendeleo yake katika ulipaji,” alisema Sylver na kuongeza;

Jackline Wolper.

“Mwingine ni msanii mahiri wa kughani mashairi, Mrisho Mpoto ambaye tulikuwa tukimdai karibu milioni 34 lakini naye ameshaanza kulipa na taratibu anakwenda kumaliza deni lake. “Kuna msanii mmoja wa Bongo Fleva anayemiliki kampuni ya muziki ambaye naye tulikuwa tukimdai milioni 74 na baada ya kumpa kibano ameweza kulipia kwa awamu na hadi sasa ameshafanikiwa kupunguza kama milioni 53.

Nay wa Mitego.

WENGI WAO KUFUNGIWA

Sylver alipigilia msumari kuwa hawataacha kuwafungia wale watakaobainika kukwepa kodi kama walivyoanza kuwafungia wengine na baada ya kuanza kulipa wakawafungulia. “Hao ni wachache tu, lakini wapo wengi ambao kwa sasa kuna timu maalum inawafuatilia na tukibaini kuwa wanaendesha kazi zao kwa ujanjaujanja na kuficha juu ya wanachokifanya, ni lazima mkondo wa sheria ushike hatamu yake.

Mrisho Mpoto.

 

 

“Tena kuna wasanii wengine tumesikia wanamiliki majumba hadi nje ya nchi lakini tunachohakikisha ni kulipwa kodi tu. Tuna nchi wanachama wa TRA kama Afrika Kusini ambapo ukimiliki nyumba basi ukilipia kodi kule huku kwetu hulipi lakini kama siyo nchi wanachama utalazimika kulipa kodi mara mbili na usipofanya hivyo kibano palepale.”

MASTAA MATUMBO JOTO!

Baada ya Ijumaa kuzungumza na meneja huyo kutoka mamlaka ya kukusanya mapato, iliwatafuta baadhi ya mastaa ambao wanamiliki makampuni na wengine wanaosaini mikataba mbalimbali ya kazi zao ili waweze kufungukia juu ya tamko hilo la TRA.

Ommy Dimpoz.

 

Kwa upande wa msanii wa filamu Bongo ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya Kay Entertainment, Kajala Masanja, alionesha kushtushwa na habari hiyo na kusema kuwa kama itatokea akafungua kitu au kuingia mkataba lazima alipe kodi. “Sina tatizo na TRA hata ukiangalia nalipa kodi inavyotakiwa.

 

Kama itatokea nimeingia mkataba au nimefungua kitu kingine lazima wajue siwezi kwepa,” alisema Kajala. Msanii mwingine ni Mrisho Mpoto aliyeanza kwa kukiri kudaiwa milioni 34 na TRA na kukaa nao meza moja.

Alikiba.

 

“Nchi inajengwa na kodi bila hiyo hatuwezi kujenga, kweli nilikuwa nadaiwa mamilioni hayo lakini niliwaambia ukweli kuhusu kipato changu na kwamba nitakuwa nikilipa kadiri uwezo wangu utakavyoniruhusu. “Nafahamu umuhimu wa kulipa kodi kwani inasaidia katika kuboresha huduma za kijamii kama maji, hospitali na barabara kwa hiyo usipolipa hivyo vitu haviendi sawa.

Ambwene Yesaya.

Nawashauri TRA kwa kuwa sasa tupo kwenye uongozi mpya iangalie namna ya kuwaelimisha wasanii wengi, mi’ nafanya kazi karibu na serikali inanisaidia kujifunza na kujua,” alisema Mrisho. Kuna wasanii wengi ambao wamekuwa wakimiliki makampuni, maduka, miongoni mwa wasanii hao ni Jacqueline Wolper (Wolper Stylish), Wema Sepetu (Endless Fame) na Jokate (Kidoti). Mastaa wengine wanaofanya muziki na kuingia mikataba ya kazi zao ni Nay wa Mitego, Ommy Dimpoz, AY, Ali Kiba na wengineo.

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Edward Kichere.

KUTOKA IJUMAA

Gazeti hili linaamini kwa kasi aliyokuja nayo Rais John Magufuli katika kuhakikisha kuwa kodi inalipwa na kila anayestahili, tunaamini TRA chini ya viongozi wake mbalimbali akiwemo kamishna wake mkuu, Charles Edward Kichere watatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Imeandikwa na Andrew Carlos na Boniphace Ngumije.

 

Rais Magufuli: Mwizi ni Mwizi Tu… Hata Kama ni Mzungu

Leave A Reply