Mazoezi ya kuapishwa Rais Mteule Dk. Magufuli yapamba moto Dar
Kibanda cha kitakachotumika wakati wa kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk John Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho kutwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Wananchi akiigiza kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange na mwingine akiigiza kama Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kulia), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Maangu (wa tatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick wakipiga saluti ulipokuwa unaimbwa wimbo wa Taifa wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Maofisa mbalimbali wakiwa katika kibanda cha kiapo wakipanga jinsi viongozi watakavyokaa wakati wa sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA; KAMANDA WA MATUKIO BLOG