Mbelgiji Avuta Bonge la Straika

Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick.

KOCHA Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems amesema kuwa bado hajaridhishwa na safu yake ya ushambuliaji huku akipendekeza kwa uongozi kuletewa straika zaidi ya hao aliokuwa nao sasa.

 

Safu ya ushambuliaji ya Simba hivi sasa inaongozwa na Mnyarwanda, Meddi Kagere, Emmanuel Okwi, John Bocco na Adam Salamba ambaye hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

 

Kauli hiyo aliitoa ni mara baada ya timu yake kushindwa kupata ushindi kwenye michezo miwili ya Ligi Kuu Bara walipocheza na Kagera Sugar na kufungwa bao 1-0 kabla ya kutoka suluhu na Azam FC.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Aussems alisema ni lazima safu yake ya ushambuliaji aiongezee nguvu katika msimu ujao kwa kushusha straika mwenye uwezo wa kufumania nyavu zaidi ya akina Kagere.

 

“Nimegundua upungufu mkubwa katika michezo miwili ya ligi tuliyoicheza dhidi ya Kagera na Azam, katika michezo hiyo yote wapinzani wetu waliiingia uwanjani kwa ajili ya kuzuia golini kwao.

 

“Mbinu hizo wapinzani wetu walijitahidi kufanikiwa kwa kutoruhusu goli na washambuliaji wangu wakakubaliana na hali hiyo kwa kutofunga bao lolote.

 

“Hivyo, basi katika kuisuka safu yangu hiyo ya ushambuliaji nimeona ni vema nikasajili mshambuliaji mwingine mwenye uwezo zaidi ya akina Kagere atakayeweza kuamua matokeo katika michezo migumu,” alisema Aussems.

 +255 GLOBAL RADIO UCHAMBUZI WA MAGAZETI MEI 16

Loading...

Toa comment