The House of Favourite Newspapers

Mbowe Amtaka Mchungaji Msigwa Amlipe Shil Bilioni 5 Kwa Kumchafua, Mawakaili Wake Waeleza – Video

0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe amemtaka aliyekuwa mwanachama wa chama hicho Peter Msigwa ambaye kwa sasa amehamia Chama Cha Mapinduzi(CCM) kumlipa fidia ya shilingi Bilioni tano za kitanzania (5,000,000,000/=).

Kupitia taarifa ya mahitaji(Demand notice) iliyotolewa na mawakili kutoka Matwiga Law Chambers imesema Msigwa anapaswa kumlipa Mbowe kiasi hicho cha fedha kwa kuzungumza taarifa za uongo dhidi yake na kumchafua ikiwa ni pamoja na kuharibu taswira ya Mbowe kisiasa, kidini, kirafiki pamoja na kifamilia.

Leave A Reply