The House of Favourite Newspapers

MBUNGE ‘ALITABIRI’ KUZAMA MV NYERERE “MNATAKA TUWAOMBE RAMBIRAMBI?”- VIDEO

UNAWEZA kusema ni kama alitabiri ajali ya MV Nyerere iliyotokea jana katika ziwa Victoria, ni kutokana na Mbunge wa Ukerewe (CHADEMA), Joseph Mkundi ambaye mnamo Aprili 24, 2018 (takribani miezi mitano) iliyopita alisimama Bungeni jijini Dodoma na kumuuliza swali aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wakati huo, Prof. Makame Mbarawa kuhusu ni lini Serikali itafanya ukarabati wa MV Nyerere ambayo alidai mashine zake zilikuwa na hitirafu.
“Kuna kivuko kinachounganisha kati ya Kisiwa cha Ukara na Ukerewe, kina hudumia zaidi ya wananchi 50,000, kimekuwa kikileta shida mara kwa mara, nimekuwa nikiwasiliana na wizara mara kwa mara, hatupendi kuja kuomba rambirambi kwa sababu ya wananchi kuzama kwenye kivuko kile.
“Tangu mwaka jana tuliahidiwa kwamba mpaka Desemba mashine mbili ambazo zilikuwa zimeagizwa zingekuwa zimeshafungwa lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea. Niombe kauli ya serikali, ni lini mashine hizo zitafungwa ili kivuko hicho kitoe huduma katika mazingira ya usalama.

Aidha, zoezi la uokoaji wa abiria waliokuwemo katika kivuko cha MV Nyerere kilichozama lilisitishwa jana usiku kutokana na giza na litaendelea tena leo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amesema mpaka sasa watu waliookolewa wakiwa hai ni 37 na waliopoteza maisha ni 44.

VIDEO: MSIKIE MBUNGE HUYO AKIFUNGUKA

Comments are closed.