Meneja: Ajibu Anakwenda TP Mazembe – Video

Nahodha wa Yanga, Ibrahimu Ajibu

MENEJA wa nahodha wa Yanga, Ibrahimu Ajibu ambaye ni Athuman Ajibu amelipokea dili la mteja wake kujiunga na TP Mazembe ya DR Congo na litatiki. Ajibu ambaye ni injini ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kutoa pasi 17 za mabao na kufunga mabao sita anawindwa na Mazembe na wameshawasiliana na Yanga.

 

Akizungumza na SpotiXtra, alisema; “Ajibu amepata ofa ya kujiunga na TP Mazembe nina imani atajiunga na timu hiyo kwani malengo ya  kila mchezaji ni kutoka hatua moja kwenda nyingine hivyo ni suala la muda tu.”

“Uongozi wa Yanga, mashabiki pia wanatambua juu ya Ajibu kutakiwa na timu hiyo, hivyo tutajadili kwa pamoja ili tujue tutafanyaje kwani mteja wangu mkataba wake unamalizika tarehe 30, maamuzi yatakuwa yetu kumfanya awe mchezaji huru ama awe ndani ya Yanga,”alisema Ajibu.

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema; “Kuhusu mchezaji wetu Ajibu kutakiwa na timu ya TP Mazembe ni kweli ipo wazi na barua tumeipata hivyo  tunatarajia kufanya majadiliano na  Mazembe pamoja na mchezaji mwenyewe  ili kuona ni jinsi Sambamba

 

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA,  Dar es Salaam

KOCHA ZAHERA Athibitisha AJIBU Kuchukuliwa na TP MAZEMBE


Loading...

Toa comment