The House of Favourite Newspapers

Miaka 22 ya Uvimbe wa Ajabu

0

STORI: MAYASA MARIWATA NA GLADNESS MALYA/GPL/Uwazi

UJAFA hujaumbika! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na kijana Robert Mkunya

(30) kukumbwa na uvimbe kwenye shavu la kushoto na kupooza, baada ya kuanguka na kupoteza fahamu alipokuwa shule ya msingi.

Akizungumza na mwandishi wetu kijana huyo ambaye anateseka kwa takriban miaka 22 sasa baada ya kukumbwa na balaa hilo tangu mwaka 1995 mkoani Dodoma anasema, tatizo hilo lilimkumba akiwa shuleni anacheza mpira na wanafunzi wenzake, ghafla akasikia kizunguzungu akaanguka na kupoteza fahamu.

KIWANJANI KWENYE MPIRA Akifafanua zaidi alikuwa na haya ya kusema: “Wakati nikiwa uwanjani nacheza mpira na wenzangu nilijikuta nina kizunguzungu na kuhisi kama kuna mtu ananisukuma nikaangua, nilipoanguka niliangukia kwenye jiwe, damu zikatoka nyingi mdomoni, nikapoteza fahamu.”

“Nilipozinduka nikajikuta nimevimba shavu hapohapo mwili wangu kuanzia miguuni nikawa nimepooza.

MATIBABU HADI KWA WACHINA

“Baada ya tukio hilo nimezunguka kwenye hospitali na kupata tiba mbalimbali bila mafanikio, ikiwemo Hospitali ya Wachina ya Dodoma wakasema damu imevilia ndani.

“Wachina hao walinishauri nije Dar es Salaam kutibiwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Kutokana na ugumu wa maisha nilikaa muda mrefu bila kuwa na uwezo wa kuja lakini mwaka huu ndiyo nikafanikiwa kuja kupata tiba Muhimbili.”

NATAKIWA KUFANYIWA OPERESHENI

Akiendelea kuzungumza kwa majonzi tele huku akilengwalengwa na machozi Mkunya anasema: “Nilipofika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili niliambiwa natakiwa nifanyiwe operesheni ambayo itagharimu shilingi laki tatu sasa uwezo huo sina.

“Kutokana na hali ngumu ya maisha niliyonayo imenilazimu kupita mtaani

kuombaomba ili kuona kama nitapata hizo fedha.

Mimi masikini sina uwezo familia yangu pia ina hali duni, hapa Dar nimekuja kwa ajili ya matibabu nimefika ubungo maziwa .

Nawaomba Watanzania wenzangu wanisaidie, nimeteseka kwa kipindi kirefu, miaka 22 na ndoto zangu zote zimezimika.

Kwa yeyote aliyeguswa na tatizo la kijana huyu na anataka kumsaidia ili kufanikisha matibabu yake awasiliane kwa namba yake ambayo ni +255 682223409.

Leave A Reply