The House of Favourite Newspapers

Michezo yote 52 ya Afcon 2019 mubashara DStv

ZIKIWA zimebaki siku chache kabla ya michuano ya Kombe la Mataifa Africa (Afcon) 2019 kuanza kutimua vumbi nchini Misri, Kampuni ya MultiChoice Tanzania (DStv) imetangaza rasmi kampeni maalum kwa Watanzania itakayowawezesha kushuhudia michezo yote 52 ya mashindano hayo ambayo yatakuwa mubashara kupitia chaneli za Supersport zilizo katika mfumo wa HD.

 

Akizungumza katika hafla ya kuzindua kampeni hiyo ya DStv ijulikanayo kama ‘DStv Tupogo’ hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, Jacqueline Woiso alisema kuwa: “Tuna furaha kubwa kwa nchi yetu kupata fursa ya kushiriki katika michuano hii ya kimataifa baada ya takribani miaka 39 tangu iliposhiriki kwa mara ya mwisho mnamo miaka ya 1980.

Mhariri Mtendaji wa Global Group, Saleh Ally (kulia) akisalimiana na Shumbana Walwa.

“Na kama ilivyo ada, ni jukumu letu na la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa tunawatia moyo vijana wetu na kuifanya
nchi yetu ifanye vizuri katika michuano hii ya kimataifa.

 

“Kwa kuzingatia hilo DStv imehakikisha kuwa mechi zote 52 za michuano hii ya kimataifa ya Afcon 2019 itarushwa mubashara DStv kupitia chaneli za Supersport na kwa lugha adhimu ya Kiswahili na katika mfumo wa
HD.

Zaidi ya hayo, DStv imehakikisha kuwa mechi hizo zinaonekana katika vifurushi vyote kuanzia kile cha DStv Bomba cha Sh. 19,000 tu.

 

“Tumehakikisha kuwa mechi hizi zinakuwepo hadi kwenye kifurushi cha chini kabisa ili kuwawezesha Watanzania wengi kushuhudia mtanange huo na kuwa sehemu ya historia ya nchi yetu kwani tunashiriki baada ya zaidi ya miaka 30.

 

” Tofauti na uzinduzi huo pia ulifanyika utambulisho wa wachambuzi wa Kiswahili wa Supersport ambapo kwa mara ya kwanza mwanadada Salama Jabir ataungana na timu hiyo katika kuongeza ladha na vionjo na hivyo kuongeza burudani na msisimko wa watazamaji.

 

Wachambuzi wengine ambao watakuwepo ni Aboubakar Liongo, Ibrahim Masoud ‘Maestro’, Edo Kumwembe, Maulid Kitenge pamoja na Oscar Oscar.

 

Akielezea zaidi jinsi Watanzania watakavyopata uhondo huo, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo alisema: “Wateja wa DStv pia wataweza kupokea matangazo ya moja kwa moja kwa kupitia ‘application’ ya ‘DStv Now’kupitia katika vifaa mbalimbali ikiwemo simu ya mkononi, laptop au tablet na televisheni ya kawaida.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Dr Omar Singo alisema kuwa: “Kitendo cha DStv kuonyesha mubashara michuano hiyo ni cha kupongezwa kwani ni sifa kubwa kwa nchi yetu, serikali inathamini michango ya aina mbalimbali inayotolewa na wadau kama DStv katika kukuza michezo. hapa nchini.”

Comments are closed.