The House of Favourite Newspapers

Mimi Mars Asema Urafiki Wake na Marioo Unafanya Kazi Kuwa Rahisi – Video

0
Mimi Mars akiwa ndani ya Studio ya +255Global Radio na Global TV

MSANII wa Bongo Fleva na Muigizaji Mimi Mars amesema urafiki alionao na msanii mwenzake Marioo unafanya mazingira ya kazi ya uandishi na utayarishaji wa nyimbo zake kuwa rahisi kwani kufanya kazi na mtu aliye na urafiki wa karibu kunamfanya anakuwa Flexible.

 

Mimi Mars amefanya ngoma mbili na Marioo huku kukiwa na maneno mengi kwa mashabiki wa muziki ambao wanadai wawili hao wanauhusiano wa kimapenzi jambo ambalo amekuwa akilikanusha kwa kudai kuwa uhusiano wake na Marioo ni wa urafiki tu.

 

Kwa upande mwingine Mimi Mars amesema kuhusu matukio yanayoendelea ya mauaji kutokana na matatizo ya mapenzi ameshauri wanandoa au watu waliopo kwenye uhusiano wanatakiwa kuwa na mazungumzo ili waweze kutatua matatizo yao kuliko kukaa na vinyongo ambavyo mwisho wa siku vinasababisha mauaji.

Mimi Mars amesema anatarajia kutoa EP ya pili

 

Alipoulizwa kuhusu wasanii ambao yupo nao karibu amewataja Young Lunya, Quick Racca pamoja na Salmin Swaggz

 

Kuhusu mipango ya kazi yake Mimi Mars amesema baada ya ngoma kadhaa anatarajia kutoa EP nyingine ambayo itakuwa ni EP yake ya pili.

 

Mimi Mars amebainisha kuwa kwenye mahusiano anatamani kuwa na mwanaume mwenye Utu, mchapakazi na anayejitambua

MIMI MARS Afunguka PENZI LAKE na MARIOO – “SIO KIKI, NAPENDA Sana KUOGELEA” | BONGO 255..

Leave A Reply