The House of Favourite Newspapers

Miss Grand Tanzania Yarudi Tena

0
Miss Grand International 2016, Ariska Putri Pertiwi.

 

BAADA ya kukaa kimya kwa miaka miwili, hatimaye lile shindano kubwa la urembo lijulikanalo kama Miss Grand Tanzania limerudi tena kwa kishindo ambapo safari hii linatarajiwa kufanyika Agosti 11, mwaka huu.

 

Akizungumza na Showbiz, mmoja wa waratibu wa shindano hilo, Abrahamu Mahimbo alisema kuwa, kila kitu kinaenda sawa na kwa mara ya kwanza katika historia ya shindano hilo kubwa duniani, wanatarajia kuwa na ugeni mkubwa ukiongozwa na Mshindi wa Miss Grand International 2016, Ariska Putri Pertiwi kutoka Indonesia akiwa na kruu yake.

 

Ariska Putri Pertiwi.

 

“Hadi sasa tumepata washiriki 28 ambao tutakuwa nao hadi siku ya fainali Agosti 11 na mshindi atapata tikiketi ya moja kwa moja kuingia katika fainali zitakazofanyika Vietnam kwenye Ukumbi wa Vinpearl Phu Quoc Resort & Villas Convention.

 

Ariska Putri Pertiwi akishika ngao ya ushindi.

 

Tunatarajia shindano la safari hii kuwa na mvuto zaidi kutokana na uwepo wa washiriki wenye sifa tunazozitaka so safari hii huenda mshindi wa Tanzania akaibuka na kuwa Miss Grand International huko Vietnam,” alisema Abrahamu.

 

SIFAEL PAUL | SHOWBIZ
 

Yajue Yaliyopo Nyuma ya Pazia, Hii Ndiyo Sababu ya Kumsaka Young Dee Akitokea Burundi

Leave A Reply