The House of Favourite Newspapers

Mke wa Wayne Rooney Atarajia Mtoto wa Nne

0
Mshambuliaji wa Everton, Wayne Rooney,akiwa na mke wake, Coleen.

Mke wa aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney, Coleen hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Twitter wenye wafuasi  milioni  1.25 amesema : “Nina furaha sana!!! ….. Sijawahi kukanusha habari hizi, lakini nilikuwa ninazilinda vyema!! Nimepimwa  na kuchunguzwa na kila kitu kiko sawa…Mtoto nambari 4 yupo njiani.”

Familia ya Rooney ikiwa katika picha na mtangazaji wa BBC.

Wayne, ambaye aliyehamia klabu ya Everton msimu huu, alisambaza ujumbe huo.

Coleen na Wayne walifunga ndoa mwaka 2008  kwa sasa wana watoto watatu wa kiume – Kai, wa miaka minane, Klay, wa miaka minne, na Kit, aliyezaliwa Januari 2016.

Katika mahojiano na jarida la New, alisema: “Nafikiria  kumpata msichana. Nina familia kubwa, kwa hivyo ningetaka wasichana sawa na ninavyowataka wavulana.”

Leave A Reply