The House of Favourite Newspapers

Mkurugenzi Manchester United Huyu Hapa

Alex Ferguson

KLABU ya Manchester United ipo katika mchakato wa kutengeneza mfumo mpya wa uongozi ndani ya klabu hiyo hasa kwenye masuala ya kiufundi.

 

Nia kubwa ya kutaka kufanya mabadiliko hayo hasa ni kumpata Mkurugenzi wa Michezo, nafasi ambayo inaonekana kuwa ndiyo mfumo wa kisasa katika klabu nyingi kubwa ili kuwarahisishia kazi makocha.

 

United inaamini ujio wa nafasi hiyo unaweza kumrahisishia kazi maneja wa timu Ole Gunnar Solskjaer hasa kuelekea mwishoni mwa msimu huu ambapo kutafunguliwa dirisha kubwa la usajili.

 

United ilikuwa moja ya klabu kubwa ambayo haina nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Michezo kwa kuwa enzi za kocha Alex Ferguson alikuwa na nguvu kubwa klabuni na hivyo nafasi hiyo haikuwa na umuhimu kwa sasa, lakini dunia imebadilika na sasa kuna mambo mengi ambayo yanailazimu klabu nayo kuingia kwenye mabadiliko.

Eric Cantona’s

Wakati mchakato wa kumpata bosi huyo ukiendelea, hawa hapa wanatajwa kuwa watu ambao wamewahi kuhusishwa au wame kuwa wote walifanya kazi pamoja kwa muda mrefu.

 

ERIC CANTONA

Kipenzi cha mashabiki wa United, jina lake linapotajwa mashabiki wa timu hiyo inayomiliki Uwanja wa Old Traff ord wanaendelea kumtambua kuwa ni shujaa wao. Cantona hayupo klabuni hapo kwa muda mrefu, lakini akirejea wengi
wanaamini atachangia kurejesha soka la kushambulia hasa kwa vijana wengi wa sasa ambao hawajui vizuri tamaduni ya klabu hiyo.

 

GARY NEVILLE
Alianguka katika uko- cha lakini bado amekuwa aki- tajwa na kuhusishwa na klabu hiyo ya United.

kuwa wakitajwa kuwa wanaweza kupewa nafasi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Man United, Ed Woodward ndiye mtu wa mwisho kufanya chaguo yupi anafaa na yupi hafai kwa cheo hicho:

Gary Neville

RIO FERDINAND

Beki na nahodha wa zamani wa timu hiyo, tayari amekutana na Woodward na kufanya mazungumzo kuhusu cheo hicho. Kwa sasa Rio ni mchambuzi wa soka na anafanya biashara zake binafsi.

 

Rio alishinda mataji mengi akiwa na Solskjaer, inaaminika wakifanya kazi pamoja wanaweza kuwa na mafanikio kwa kuwa wanaheshimiana na wanajuana vizuri kwa Neville alikuwa beki mahiri na nahodha wa timu hiyo, ana uhusiano mzuri na Solskjaer, anaweza kusaidia katika utafutaji wa wachezaji wenye ubora na uimara wa kuichezea timu hiyo.

 

FABIO PARATICI

Amekuwa mkurugenzi wa ufundi wa Juventus tangu mwaka 2010, amewaongoza kubeba mataji ya Serie A mara nane mfululizo tangu mwaka 2012. Amehusika katika kumsajili Paulo Dybala, akitua United anaweza kutoa changamoto kwenye soka la England.

 

PAUL MITCHELL

Skauti za zamani wa Tottenham na kwa sasa yupo RB Leipzig ya Ujerumani, amewasaidia klabu hiyo kushika nafasi ya pili katika msimu wao wa kwanza wa Bundesliga. Ni damu changa kwenye majukumu mazito na akipata nafasi ya kutua United anaweza kuwa na msaada mkubwa kwenye mradi wa kukuza chipukizi kutoka kwenye akademi yao.

 

JOHN MURTAGH Mkuu wa Kitengo cha Kukuza Maen
deleo wa Old Traff ord, ikitokea akapata nafasi ya kuwa mkurugenzi itamaanisha kuwa amepanda cheo. Anaijua klabu vizuri, mchango wake ni kukuza chipukizi kama alivyofanya kwa Mason Greenwood.

 

EDWIN VAN
DER SAR Mmoja wa makipa bora kuwahi kutokea kwenye soka la England, kwa sasa anafanya vizuri akiwa ni bosi wa Ajax. Amekuwa na msaada katika timu hiyo kufi ka nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu na ni kama wapo kwenye njia ya kwenda fainali ya michuano hiyo

 

PAUL SCHOLES

Bado ni kipenzi cha mashabiki wa United lakini hivi karibuni alipata nafasi ya kuwa kiongozi wa soka kwenye levo ya chini akashindwa, inawezekana hilo likachangia kushusha thamani yake ya kupewa ukurugenzi.

Alipewa majukumu ya kufundisha Oldham akashindwa na kujiuzulu ndani ya wiki chache tu tangu apewe majukumu. Scholes hana nafasi kubwa ya kupewa nafasi hii kwa kuwa amekuwa mzungumzaji mzuri kwenye vyombo vya habari hata kama ni dhidi ya kikosi hicho cha Solskjaer.

MICHAEL ZORC

Nguli wa Dortmund, huyu inaweza kuwa ngumu kuondoka klabuni kwake kwa sasa kwa kuwa licha ya kazi lakini pia ni klabu anayoipenda. Ni mtu mzuri kwenye masuala ya kibiashara, anaweza kuisaidia United kupata chipukizi bora kama alivyofanya kwa Jadon Sancho.

 

PETER SCHMEICHEL

Kipa bora wa United katika historia, anasifika kwa kubeba mataji mengi, huyu alishawahi kuweka wazi kuwa anaitamani nafasi hiyo ya ukurugenzi Akipewa nafasi, kwa kuwa anaijua klabu vizuri huku pia akiwa amewahi kufanya kazi kwa ukaribu na Solskjaer wanaweza kuwa na muunganiko mzuri.

Comments are closed.