MOBETO AKIENDEKEZA MITANDAO ATAJIKONDESHA

Modo ambaye kwa sasa anafanya poa kwenye Bongo Fleva,Hamisa Mobeto, ‘Misa’ amefunguka kuwa akiwa anafuatilia kila kinachoandikwa kuhusu yeye kwenye mitandao ya kijamii atakuwa anajikondesha tu. Misa ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa ili maisha yaendelee vizuri kama kawaida ni kutofuatilia kila kinachoandikwa kwenye mitandao maana kutamfanya kushindwa kuendelea na mambo yake muhimu ya kimaisha.

“Nikisema nifuatilie kila kitu kinachoandikwa mitandaoni, itanitesa na kunifanya nikonde na kubaki mifupa mitupu bila sababu za msingi hivyo sasa hivi siyapi nafasi kabisa mambo ya mitandaoni,” alisema Misa.


Loading...

Toa comment