The House of Favourite Newspapers

Molinga, Moustafa Wakwama CAF, Kuwakosa Pyramids ya Misri

David Molinga raia wa DR Congo.

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa utaendelea kuwakosa nyota wake wawili wa kimataifa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na kubanwa na kanuni za shirikisho hilo.

 

Yanga itamkosa mshambuliaji wake, David Molinga raia wa DR Congo na beki Mustafa Seleman raia wa Burundi katika mchezo wa mtoano dhidi ya Pyramids ya Misri utakaopigwa Oktoba 27, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema kuwa: “Naomba niweke sawa katika suala la Molinga na Moustafa kwamba wachezaji wetu hawa hawatokuwa sehemu ya kikosi chetu kitakachocheza na Pyramids kwa kuwa kanuni za Caf zinatubana.

 

“Katika hatua hii hawatoweza kucheza hata kama bado tungekuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ingekuwa hivyo lakini kama kule tungefuzu makundi basi tulikuwa na uwezo wa kuwatumia na hata huku tukifuzu basi watatumika kwenye hatua ya makundi,” alisema Mwakalebela.

Comments are closed.