×

Mondi Amrudisha Aunt kwa Iyobo

 

MSANII Nasib Abdul ‘Diamond’, ni kama amejipa kazi ya kuwapatanisha dansa wake Mose Iyobo na staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel, ambao mahaba yao yalichacha hivi karibuni.

 

Diamond ambaye ni bosi wa Lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, alimwambia staa huyo wa fi lamu kwamba, “Lazima atarudi kwa Mose Iyobo”.

 

Msanii huyo aliyasema hayo hivi karibuni kwenye sherehe ya Maulidi ya dada yake, Esma Khan, iliyofanyika nyumbani kwa mama yao Madale, ambapo Aunt na Iyobo walikuwa sehemu ya waalikwa.

 

“Unajifanya sasa hivi hutaki kutusikia, lakini ukweli ni kwamba, hakuna pa kukimbilia, ni lazima utareje kwa mzazi mwenzako (Moses Iyobo),” Diamond alimwambia Aunt kwa sauti, huku waalikwa wengine wakisikia na kuangua kicheko.

ISHU ILIANZA HIVI

Aunt alikuwa ameketi kivyake na waalikwa wengine, ghafla Diamond alimjongea na kuanza kumpa vijembe hivyo huku Mose Iyobo aliyekuwa nyuma yake akisikia.

 

“Mimi nachojua wewe ni shemeji yetu, haijalishi chochote nenda weee huko; zunguka uwezavyo lakini hapa (kwa Mose) lazima urudi kwa vyovyote vile hata kama waarabu (haijulikani ni wepi) wamekuteka,” alisema Diamond na kumfanya Mose Iyobo kuangua kicheko.

 

Wakati Diamond akimpa vimipasho vya ushemeji, Aunt naye alikuwa akitabasamu huku akimtupia jicho Mose Iyobo ambaye alikuwa nyuma ya Diamond.

 

“Mbona huyo mtu (Mose Iyobo) amejifi cha, sasa si ajitokeze tu,” alisema Aunt huku akicheka, kitendo kilichotafsiriwa na baadhi ya watu waliokuwepo pale kuwa jamaa bado wanapendana.

 

Aunt na Iyobo waliishi pamoja kama mke na mume kwa takriban miaka miwili bila kufunga ndoa na kufanikiwa kupata mtoto wa kike aitwaye Cookie.

 

Aidha, mambo yalipokuwa mengi, wawili hao walipeana kisogo, huku Aunt akidaiwa kuanzisha uhusiano mpya wa kimapenzi na kijana ajulikanaye kwa jina la Kusah ambaye pia anatajwa kumpachika ujauzito staa huyo wa filamu.

Stori: Imelda Mtema, Amani

Leave a Comment