The House of Favourite Newspapers

Montana Asema Yeye na Khloe Kardashian Bado Marafiki

 

French Montana Denies Cheating on His Ex with Khloe Kardashian Amid Jordyn-Tristan Scandal

RAPA kutoka pande za Marekani, Karim Kharbouch, maarufu kama French Montana, amezidi kuweka mkazo kuwa yeye na Khloe Kardashian ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani  bado ni marafiki.

Montana na Kardashian waliaanza mahusiano yao mwaka 2014 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya mrembo huyo  kuachana na mpenzi wake Lamar Odom.  Mahusiano yake na Montana yalidumu kwa miezi mitano.

Rapa huyo amefunguka  kwamba kuachana kwao hakukuwa kwa ugomvi, hivyo watabaki kuwa marafiki kwa kuwa ni marafiki wakubwa na hakuna ambaye alikuwa na kinyongo na mwenzake.

“Ninaamini uhusiano wetu ulikuwa wa kweli, hapakuwa na tatizo lolote kati yetu, hakuna ambaye alimfanyia kibaya mwenzake na kusababisha kati yetu tushindwe kuwa pamoja kwa namna yoyote,” alisema Montana.

Comments are closed.