MREJESHO BAADA YA KUUJARIBU UCHAWI WA ‘CHUMA ULETE’
BAADA ya kusikia simulizi mbalimbali kuhusiana na ‘chuma ulete’ kwa muda mrefu, nikaamua nijaribu ili niweze kurahisisha maisha. Nilitamani sana zile hadithi za ‘chuma ulete’ ziwe kweli juu yangu. Ninunue bidhaa kisha fedha zinirudie, zikiwa nyingi zaidi. Nile bila jasho.
Baada ya mawazo hayo, siku chache zilizopita nikaamua kwenda kwa mganga mmoja wilayani Bagamoyo ambaye alisifika kwa kutengeneza utaalamu huo.
Nilifika kwa mganga, nikavua viatu kisha nikaingia ndani. Kama kawaida mganga alinikaribisha kwa mapambio ya ‘kilozi’. Zilipigwa chafya nyingi zilizosindikiza maneno yasioeleweka.
Kabla sijamweleza shida iliyonipeleka pale, mganga akaanza kubashiri: “Kijana una matatizo makubwa, mambo yako hayaendi kuna watu wanakuchezea… umekuja kumtambua anayekufanya ushindwe kupiga hatua… ”
Mganga mtaalamu, mlozi aliendelea kuongea mambo mengi ambayo sikuhusiana nayo, nilipoona anazidi kupotea, nikamweleza shida iliyonipeleka: “Mzee nimekuja kwa shida moja tu, nataka unipe uchawi wa chuma ulete, nipate pesa bila jasho.” SOMA ZAIDI
[…] nini Samike hakumtibu binti yake? Umesema alikuwa mchawi haijapata kutokea,” […]