Msaidizi Wake Afichua Siri Nzito ya Mariah Carey

MWANAMUZIKI Mariah Carey ana makalio ya bandia, hii imethibitishwa na aliyekuwa msaidizi wake Lianna Shakhnazarryan kwenye mgogoro wao wa kisheria unaoendelea.

 

Imeelezwa kua, baada ya Carey kumburuza mahakamani Lianna kwa madai ya kumtishia kuvujisha picha zake chafu, Lianna naye alimfikisha mahakamani Carey akidai kuwa ni wizi wa fedha uliofanyika kwenye akaunti yake ya benki ambapo Carey alichukua pesa na kwenda kufanyia upasuaji wa makalio yaani Plastic Surgery.

 

Kwa mujibu wa Daily Mail, Lianna ameieleza mahakama kwamba Maria alichukua Card yake ya benki na kwenda kutoa pesa akitumia jina la (Stella Carey) na kuchota kiasi cha dola 10,000 kwa kwa ajili ya upasuaji huo, pia alikomba dola 4,800 kwa ajili ya kunenepesha matiti na dola 8,900 kwa ajili ya kutengeneza shingo yake na sehemu za taya.


Loading...

Toa comment