The House of Favourite Newspapers

Mshindi wa Kubashiri Soka wa Premier Bet Alamba Mamilioni ya Pesa

Mshindi  wa Premier Bet, Andrea Elias Sebastian (kushoto) mkazi wa Wilayani Igunga mkoani Tabora akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo.
Mshindi  wa Premier Bet, Andrea Elias Sebastian (kushoto) mkazi wa Wilayani Igunga akikabidhiwa hundi ya mamilioni yake.
Akipeana mkono na viongozi wa Kampuni ya Premier Bet wakati wa hafla hiyo.
Hafla ikiendelea kwa mshindi wa mamilioni.

Kampuni ya Kubashiri Soka ya Premier Bet Tanzania imemtambulisha  mshindi wa kubashiri soka ambaye ni Andrea Elias Sebastian mkazi wa Wilayani Igunga mkoani Tabora ambaye ameibuka na zaidi ya shilingi milioni 53 baada ya kubashiri kwa usahihi.

 

Mshindi wetu alicheza mchezo wa kubashiri soka maarufu kama Sports Betting (SB) katika tawi letu la Igunga mnamo tarehe 18/10/2019. Akiwa amechagua timu 38 kwa dau la shilingi elfu moja (1,000/=)tu, mshindi wetu alifanikiwa kutabiri sahihi mechi zote 38 na kushinda kitita cha Shilingi Milioni hamsini na  tatu laki sita thelathini na sita na mianane na arobaini na moja (53,636,841/=) taslimu.

 

Uongozi wa kampuni ya Premier Bet,umempongeza mshindi,  Andrea Elias Sebastian kwa ushindi huu mnono na kufurahia kumkabidhi hundi ya kiasi cha Milioni hamsini na tatu laki sita thelathini na sita na mia nane na arobaini na moja (53,636,841/=) taslimu kama malipo ya ushindi wake mbele ya waandishi wa habari makao makuu ya ofisi zao jijini Dar es Salaam.

 

Wakati wa hafla hiyo ya kumkabidhi pesa zake za ushindi, Andrea alisema “Ninafuraha sana kushinda fedha hizi nyingi zitakazoenda kubadilisha maisha yangu. Nilikuwa nashauku kubwa sana baada ya kufuatilia matokeo ya mechi moja baada ya nyingine, baada ya kugundua kuwa kubashiri sahihi matokeo ya mechi zote 38 nilihisi ni mtu mwenye furaha dunia nzima”.

Wakati wa hafla  hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Premier Tanzania Bw. Sami Matar alisema “Tunayo furaha kumkabidhi hundi mshindi wetu na tunajivunia kusema kuwa Premier Bet ni kampuni inayolipapesa kwa haraka zaidi wa shindi wetu. Tunamtakia, Andrea kuendelea kuwa mwenye bahati maishani mwake mwote.”

 

Kampuni yetu ya Premier Bet inapenda kutoa rai kwa watanzania wote nchini wenye umri zaidi ya miaka 18 kuhamasika na ushindi huu kwa kuendelea kubashiri na kampuni yetu ya Premier Bet kwakupitia mawakala wetu, maduka yetu na mtandaoni. Tunapenda kuwafahamisha kwamba Premier bet ni kampuni thabiti inayotoa malipo kwa haraka na uhakika mara baada ya ushindi. Kima cha chini cha ubashiri na Premier Bet Tanzania ni shilingi mia mbili (200/=) mtandaoni na miatano (500/=) madukani na kwa mawakala, kiwango cha juu cha ushindi ni shilingi milioni miambilithelathini na nane 238.

Mwisho, Tunapenda kufikisha dhana ya ubashiri wa kistaarabu kwa jamii yote, Tunapenda jamii itambue kuwa michezo ya kubashiri ni michezo ya kujifurahisha tu na sio chanzo cha mapato.
Kwa pamoja tunasema “BASHIRI NA WABABE”.

Comments are closed.