Msomaji: Betika limenipa Sh milioni tatu

MSOMAJI wa muda mrefu wa Gazeti la Betika, Samora Magaya mkazi wa Lindi, amefunguka kuwa, gazeti hilo limemfanya ashinde kiulaini Sh milioni tatu.

Mgaya aliyasema hayo alipokutana na timu ya maofisa masoko wa Global Publishers ambayo huingia mtaani kila Jumatano wakati gazeti hilo linapoingia mtaani.

Jana Jumatano, timu ya maofisa masoko wa Global Publishers ilitembelea Ubungo, Mwenge, Mnazi Mmoja, IFM, DIT na maeneo kadhaa ya Jiji la Dar es Salaam na kukutana na baadhi ya wasomaji akiwemo Magaya.

Akizungumzia gazeti hilo, Magaya alisema: “Mimi ni mfanyabiashara, tangu nifike Dar nimekuwa nikijihusisha na masuala ya kubeti, hili gazeti si mara ya kwanza kupata nakala yake.

 

 

“Kupitia hili nishawahi kupata Sh milioni tatu. Nawahamasisha wengine walisome kwa wingi gazeti hili ni bora sana kwa sababu linakupunguzia muda mrefu wakati wa kubeti na kukuongezea kipato.”

Naye Ayoub Salum, alisema Gazeti la Betika linawahabarisha wananchi juu ya masuala ya michezo ya timu mbalimbali za soka.

“Gazeti hili linarahisisha mambo kwani kwa wale watu wa kubeti hivi sasa hawana haja ya kwenda kwenye zile sehemu maalum zilizowekwa za kubetia, badala yake ukiwa na gazeti lako popote pale unamaliza kazi yako,” alisema Salum.

Gazeti hilo ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na linaingia mtaani kila Jumatano.

Betika lenye kurasa 20 za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.

Bado kuna nafasi za kutangaza na Betika ambapo kwa yeyote anayehitaji kutangaza na gazeti hilo anakaribishwa ofisini Sinza Mori jijini Dar.

 

Na Mwandishi Wetu

Loading...

Toa comment