The House of Favourite Newspapers

Mtambo wa Mabao Azam Waahidi Kazikazi msimu ujao wa 2024/25

0
Adam Adam ambaye ni mshambuliaji mpya wa Azam.

INGIZO jipya ndani ya Azam FC, Adam Adam ambaye ni mshambuliaji ameweka wazi kuwa amerejea ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kufanya kazi hivyo mashabiki wategemee makubwa.

Ni Juni 6 2024 Azam FC walimtambulisha mshambuliaji huyo kuwa ni mali yao kwa kandarasi ya mwaka mmoja hivyo atakuwa kwenye anga la kimataifa ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nyota huyo kwa msimu wa 2023/24 alikuwa anacheza ndani ya Mashujaa ya Kigoma alifunga jumla ya mabao 7 msimu ujao wa 2024/25 atakuwa kwenye timu iliyomkuza Azam FC.

Adam amesema: “Nimerejea nyumbani kuja kufanya kazi, wategemee mazuri nimekuja kazini. Nimefurahi kurejea nyumbani hivyo kazi itafanyika.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi tunaamini kwamba tutafanya vizuri kwenye mashindano ambayo tunashiriki. Kikubwa ushirikiano pamoja na kufanya kazi kwani hilo linawezekana.”

Kumaliza nafasi ya pili kwa Azam FC ikiwa na pointi 69 inaungana na Yanga ambao ni mabingwa wa ligi kupeperusha bendera kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka, GPL

Leave A Reply