The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Chacha Wangwe Anusurika Kifungo, Alipa Faini (Video)

0
Bob Chacha Wangwe (mbele) akiongea na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kulipiwa faini ya Sh. milioni tano na baba yake mkubwa, Prof. Samuel Wangwe.
…Akiendelea kuzungumza na waandishi wa habari.
…Akitoka chumba cha mahabusu baada ya kulipiwa faini.
…Akiwa na mawakili wake.

MAHAKAMA ya Kisutu imemhukumu Bobo b Chacha Wangwe kwenda jela mwaka mmoja na nusu au kulipa faini ya Sh. Milioni 5 kwa kupatikana na hatia ya kuchapisha taarifa ya uongo Facebook alikoandika: “Haiwezekani Znz kuwa koloni la Tanzania Bara kwa sababu za kijinga”.

Habari kutoka mahakamani zinasema ndugu wa Wangwe wanachanga fedha hizo ili kumnusuru na adhabu ya kwenda jela.  Hata hivyo, baada ya kuchangwa kwa fedha hizo, baba yake mkubwa, Prof. Samuel Wangwe, alirejea katika mahakama hiyo akiwa na risiti ya malipo ya faini hiyo na hivyo kumfanya Bob kuwa huru na kuondoka mahakamani hapo.

STORI: DENIS MTIMA, GPL

Leave A Reply