The House of Favourite Newspapers

Mwakyembe Alivunja Baraza la Michezo kwa Agizo la Waziri Mkuu

0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na wanahabari.

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, leo Julai 10 amesitisha uteuzi wa mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuanzia leo kwa mamlaka aliyopewa na sheria ya BMT Na.12 ya 1967.

 

Mwakyembe ameeleza kuwa sababu ya kusitisha uteuzi huo inatokana na agizo alilopewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyemwagiza afanyie kazi mapitio na kulitathmini upya baraza hilo ili kujiridhisha na usimamizi wake kuhusu michezo.

 

Kutokana na kujiridhisha kwake kwamba usimamizi wa BMT si imara, amelivunja na ataliunda upya. Kwa sasa sekretarieti ya baraza hilo itaendelea kufanya kazi katika kipindi hiki ikishirikiana na wizara.

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

LIVE: Rais Magufuli Apokea Nyumba 50 za Mkapa Foundation -Chato

Leave A Reply