The House of Favourite Newspapers

KASHASHA: Chama Hatadumu Simba, Anacheza Mpira wa Majukwaa – Video

MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Alex Kashasha,  ameichambua mechi ya Ligi Kuu kati ya Simba na Mtibwa Sugar iliyochezwa jana Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kusema mchezaji Clatous Chama hawezi kudumu Simba kwa sababu anacheza mpira wa majukwaa wa kujionyesha kwa mashabiki, hivyo akikosolewa atachukia.

 

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, hivyo  kuirejesha kileleni kwa kuishusha  Yanga ambayo ilikuwa inaongoza  baada ya kufikisha jumla ya pointi 83 huku Simba ikifikisha jumla ya pointi 85.

 

Simba wana pointi 84 na mabao 72, kinara wa mabao akiwa ni Meddie Kagere mwenye mabao 20.

 

Timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, jijini Dar es Salaam ina michezo minne mkononi ili kukamilisha ligi ya msimu huu, ikitakiwa kuwa na pointi tano ili kutetea ubingwa wake.

MSIKIE KASHASHA

Comments are closed.