The House of Favourite Newspapers

Mwanamke Aeleza Alivyobakwa Na Chris Brown

 

MSANII wa Marekani,  Christopher Maurice Brown maarufu kama Chris Brown,  anaandamwa na tuhuma za kumbaka mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 24 huko Ufaransa usiku wa Januari 15 mwaka huu.

 

Mwanamke huyo amesema kwamba alifanyiwa tukio hilo baada ya kukutana na msanii huyo club huko ufaransa, na akamkaribisha chumbani kwenye hoteli aliyofikia iliyokuwa inajulikana kwa jina la ‘Mandarin Oriental Hotel.Mwanamke huyo amefunguka kwamba chumba walichotumia na Chris Brown ndipo alipomfanyia kitendo hicho  humo.

 

Chris Brown (Breezy) hajasema neno lolote juu ya taarifa hizo.

 

Taarifa zilizotolewa na chanzo cha Ufaransa cha  ‘Closer’,   kinaeleza kwamba Breezy yupo chini ya upelelezi wa polisi kuhusiana na tuhuma hizo.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.