Mwanasheria mkuu wa kwanza wa raia wa Kenya bwana Charles Njonjo amefariki dunia akiwa na miaka 101.
Rais Uhuru Kenyatta ametangaza leo Jumapili, Januari 2, 2022 taarifa ya kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe Charles Mugane Njonjo.
“Ni kwa masikitiko makubwa kwamba asubuhi ya leo, Jumapili tarehe 2 Januari 2022, nimepokea taarifa za kuhuzunisha na za kufariki kwa Charles Mugane Njonjo,” Rais Kenyatta amenukuliwa na magazeti ya Kenya.

Njonjo, alikuwa mjumbe pekee aliyebaki katika Baraza la Mawaziri la uhuru wa Kenya.
Kufariki kwa Mhe. Njonjo ni pigo kubwa sio tu kwa familia yake bali kwa Wakenya wote na kwa hakika, bara zima la Afrika kwa sababu ya jukumu lake kuu katika kuanzishwa kwa taifa la Kenya wakati wa uhuru,” Rais alisema.
keny
Taarifa kutoka kwa familia zinasema, maiti ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Charles Njonjo tayari imechomwa katika mji wa Kariokor jijini Nairobi.
