MWIJAKU AMKALIA KOONI BATULI

BAADA ya mnyukano mzito wa maneno yasiyofaa kwenye mitandao ya kijamii kati ya msanii wa filamu za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ na mwenzake, Mwemba Batoni ‘Mwijaku’, bado mambo ni moto.  Vita ya maneno ingali ikiendelea kwa wasanii hao ambapo Mwijaku amezidi kumkalia kooni Batuli na kupuuza kitisho cha kupelekwa mahakamani kwa lugha zisizofaa ambapo amesisitiza kuwa hajutii kile alichokisema.

Awali Mwijaku kupitia chombo kimoja cha habari alisema, Batuli ni msanii wa mtaani na ameingia kwenye sanaa ya filamu kwa ajili ya kufanya mambo yasiyofaa.Kauli hiyo ilimuudhi Batuli na kujikuta akimjibu maneno ambayo hayafai kukaririwa kwenye gazeti na baadaye kutishia kumpeleka Mwijaku mahakamani kwa kumtolea maneno machafu. Hata hivyo, Mwijaku alipohojiwa na mwandishi wetu aliyetaka kujua anakichukuliaje kitisho cha kupelekwa kortini ambapo alisema:

“Kamwe siwezi kutengua kauli yangu kwa sababu huo ndiyo ukweli. “Nasisitiza Batuli ni msanii wa mtaani, hebu niambieni mara ya mwisho kumuona ametoa kazi ni lini? “Yupoyupo tu na huo ndiyo ukweli, maana sanaa hii ninaijua vizuri na iko kwenye damu. “Kama ni mahakamani aende kwa kuwa nami najua sheria vilevile, nimeongea kitu halisi siyo cha kutunga,” alisema Mwijaku. Alipotafutwa Batuli ili kujua kama ameshaanza taratibu za kumfikisha msanii mwenzake mahakamani, hakupatika.


Loading...

Toa comment