The House of Favourite Newspapers

Mwijaku Apewa 21 Kuwasilisha Utetezi wake Mahakamani

0
Mtangazaji Burton Mwemba (Mwijaku)

Mahakama Kuu masjala ndogo ya Dar es salaam leo Septemba 3, 2024 kupitia kwa Jaji David Nguyale imetoa siku 21 kwa mtangazaji Burton Mwemba (Mwijaku) kuwasilisha utetezi wake mahakamani.

Mwijaku alifunguliwa kesi ya madai na Ally Masoud (Kipanya) akitakiwa kumlipa Bilioni 5.5 kwa madai ya kumkashifu kupitia mitandao ya kijamii.

Wakili wa Mwijaku, Peter Maleo ameiomba mahakama kuongeza muda ili aweze kuwasilisha utetezi wake kwa njia ya maandishi kujibu madai ya Kipanya.

Kipanya amefungua kesi hiyo ya madai namba 18911 ya Agosti 5, 2024 akiomba nafuu 12 ikiwamo kulipwa fidia kwa kukashifiwa mtandaoni na Mwijaku.

BUNGENI: WABUNGE WANATOA HOJA NZITO KUTETEA MASLAHI YA WANANCHI WAO – DODOMA…

Leave A Reply