Mwili wa Marehemu Jenista Mhagama Waagwa Dodoma, Mazishi Desemba 16 Peramiho – (Picha +Video)

Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma, marehemu Jenista Joakim Mhagama, umeagwa rasmi leo Desemba 13, 2025 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kiwanja cha Ndege, Jijini Dodoma, katika ibada iliyoongozwa na viongozi wa dini.
Ibada hiyo ya kuaga imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba, Spika wa Bunge Mussa Azzan Zungu, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Serikali, Chama cha Mapinduzi (CCM), wabunge, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu.
Akizungumzia wasifu wa marehemu, viongozi na waombolezaji wamemtaja Jenista Mhagama kuwa kiongozi aliyekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya jimbo lake na Taifa kwa ujumla, hususan katika masuala ya uwakilishi, usimamizi wa rasilimali za umma na ustawi wa jamii.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na familia, mwili wa marehemu utazikwa Desemba 16, 2025 katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma, ambako wananchi wanatarajiwa kumpa heshima za mwisho kiongozi wao.
Taifa linaendelea kuomboleza kumpoteza mmoja wa viongozi wake waliolitumikia Bunge na wananchi kwa uaminifu.


