The House of Favourite Newspapers

NABII ‘MTOTO’ ATIKISA DAR, ANA MIAKA 22, UTAJIRI WAKE UNATISHA – VIDEO

Nabii Daniel Daniel Shillah akishuka kwenye gari.

KILA kukicha wanatokea manabii wanaokuja na staili mbalimbali za mahubiri na miujiza ya kila aina, wakati Nabii Tito ambaye alikuwa akihubiri mitaani kwamba kuzini na kulewa siyo dhambi akisota Hospitali ya Mirembe mkoani Dodoma baada ya kuonekana kwamba ana matatizo ya akili, mwingine aliyetambulika kwa jina la Daniel Daniel Shillah (22), ameibuka na kutikisa Jiji la Dar.

 

Akiwa katika pozi.

 

Nabii huyo mtoto ambaye ni gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kugawa pesa kwa waumini wanaosali kanisani kwake, anaongoza kanisa linalojulikana kwa jina la Bethel International Ministry of Tanzania lililopo kwenye Viwanja vya Sabasaba na Kigamboni kwa jijini Dar na matawi Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Zanzibar, Kigoma, Morogoro na mingineyo.

 

 

Baada ya kuwepo kwa tuhuma nzito za kuwa na utajiri mkubwa usiokuwa na vielelezo, kuhusishwa na Freemasons na masuala ya utapeli kwa wanaohitaji huduma zake za maombezi, Ijumaa Wikienda liliamua kumsaka Nabii Shillah.

 

AFUNGUKIA SKENDO YA FREEMASON

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Nabii Shilla alianza kwa kufungukia skendo ya kuwa Freemason ambapo alisema siyo kweli na huo ni uzushi kwani hata hajua hao watu wanapatikana sehemu gani.

 

Akifanya mahojiano na waandishi wa Global Publishers, Sifael Paul (kulia) na Gladness Mallya.

 

“Nilianza kuhusishwa na Freemasons muda mrefu, lakini hata sijui mahali walipo,” alisema Nabii Shillah.

 

Kuhusu suala la utajiri wa kutisha, Nabii Shillah alisema kwamba hana utajiri wa kutisha kiasi hicho kama watu wanavyomzungumzia bali ana maisha ya kawaida na tofauti na utumishi wa Mungu pia amekuwa akijishughulisha na biashara mbalimbali pamoja na kilimo.

 

“Siri ya mafanikio niliyonayo ni kujituma katika kufanya kazi. Nazewa kusema siri za mafanikio zipo tatu. Moja ni kufanya kazi, ya pili ni kufanya kazi na ya tatu ni kufanya kazi.

 

Nabii Daniel Daniel Shillah.

 

“Pia siri nyingine ni kumuomba Mungu hivyo ninawasihi vijana wafanye kazi kwa bidii, waachane na kukaa tu bila kujishughulisha.

 

“Wanaosema mimi ni Freemason wana wivu tu kutokana na mafanikio yangu, lakini siyo kingine, kiukweli nilianza kumtumikia Mungu tangu nikiwa mdogo kwa hiyo nina karama ya aina yake.

 

Mtu akiwa anaumwa, ninaoneshwa anaumwa nini na nikimuombea anapona, watu wamepona sana Virusi Vya Ukimwi kanisani kwangu,” alisema Nabii Shilla.

 

Akishuka kwenye gari.

 

KUGAWA PESA KANISANI

“Huwa NInawapa pesa waumini wangu wale ambao hawana uwezo maana unakuta wengine hawana kazi, sasa kwa kuwa Mungu amenibariki, name ninagawana nao na kila Jumapili kanisani kwangu kunakuwa na chakula kwa ajili ya waumini na hata Jumapili hii (jana) nitafanya hivyo.”

 

 

NI TAPELI?

Kufuatia madai ya mmoja wa watu waliohitaji huduma kwa Nabii Shillah aliyeko nchini Marekani kisha akadai kutapeliwa na nabii huyo baada ya kumtaka amtumie kwanza kiasi cha fedha na alipotuma mpaka leo hajawahi kumuombea, nabii huyo alisema siyo kweli na hao wanaojitokeza na kumsema vibaya wanataka tu kumchafua na huduma yake.

Akiwa sehemu tulivu.

“Kama kuna mtu ambaye nilishawahi kumtoza pesa ili nimuombee au nimepokea pesa yake sijamuombea, naomba ajitokeze hadharani niko tayari, mimi kanisani kwangu sitoi kipaumbele kwenye sadaka bali ni kwenye kuwalisha watu neno la Mungu na wanaoumwa kupona tu maana Mungu ameniita kwa ajili hiyo,” alisema Nabii Shillah na kuongeza:

 

“Ninachojua ni kwamba mtu huyo aliombwa na mmoja wa wachungaji wangu achangie gharama za urushwaji tu wa matangazo kwenye runinga.”

STORI: Gladness Mallya na Sifael Paul, IJUMAA WIKIENDA

 

Mfahamu Nabii Mtoto Anayegawa Pesa Kanisani Kwake!!

Comments are closed.