The House of Favourite Newspapers

Nafasi za Kazi: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Yatangaza Nafasi 320

0

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imetangaza nafasi 320 za kazi kwa vijana wa Kitanzania wenye umri usiozidi miaka 30. BONYEZA HAPA KUZIONA

Nafasi hizo zilizotangazwa kufuatia tangazo lililotolewa na Takukuru ni maofisa upelelezi nafasi 220 na nafasi 100 za wapelelezi wasaidizi daraja la tatu.

Tangazo hili limekuja ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Polisi kutangaza nafasi 500 za ajira na watu 50,000 kujitokeza kuwania nafasi hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Takukuru  Jumamosi, Januari 21, 2023, waombaji wa nafasi ya maofisa upelelezi wanatakiwa kuwa na Astashahada au shahada ya kwanza katika kozi ya uhandisi, usanifu, sayansi ya kompyuta, sheria na saikolojia.

Kwa upande wa wapelelezi wasaidizi daraja la tatu, wanaohitajika ni waliohitimu elimu ya sekondari na mafunzo yoyote yanayotambulika ikiwemo ya ufundi kutoka katika taasisi zinazotambulika.

Mwisho wa kutuma maombi ni Februari 10, 2023 BONYEZA HAPA KUZIONA

MBOWE: RAIS SAMIA ALIKUA MVUMILUVU, MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI!

Leave A Reply