The House of Favourite Newspapers
gunners X

Naibu Waziri aagiza tathmini ya kina kuhusu uendeshaji wa Kituo cha Mabasi Magufuli

0

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Reuben Kwagilwa, ameagiza kuundwa kwa timu maalum itakayofanya tathmini ya kina kuhusu uendeshaji wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli, hususan katika kufuatilia utekelezaji wa malengo ya awali ya mradi pamoja na mwenendo wa ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza Desemba 23, 2025 baada ya kutembelea na kukagua kituo hicho, Kwagilwa alisema licha ya kituo hicho kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 54.5, bado hakijafikia matarajio ya serikali na wananchi, huku idadi ya mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi yanayotumia kituo hicho ikiwa ndogo.

“Timu hiyo itatathmini mradi huu kulingana na malengo yake ya awali, kuangalia ufanisi wa uendeshaji, miundombinu, huduma zinazotolewa pamoja na mapato yanayopatikana au kupotea tangu kituo hiki kikabidhiwe kutoka Jiji la Dar es Salaam kwenda Halmashauri ya Ubungo,” alisema.

Aidha, ameelekeza kuwa ndani ya siku 90 timu hiyo iwasilishe ripoti kamili yenye mapendekezo mahsusi ya namna ya kuboresha uendeshaji wa kituo hicho ili kiweze kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi na kuongeza mapato ya serikali.

Timu hiyo itahusisha wadau kutoka taasisi mbalimbali pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na itahakikisha changamoto zote zinazoathiri matumizi kamili ya kituo hicho zinabainishwa na kupatiwa ufumbuzi.

KESI YA LISSU SINTOFAHAMU,DPP KWANINI KIMYA?-HECHE AHOFU CHAMA KUFUTWA!-KUHUSU MUUNGANO

Leave A Reply