The House of Favourite Newspapers

Ndayiragije Avuna mil 180 Azam

FUNDI ni fundi tu. Ettiene Ndayiragije amesaini Azam Fc na jana ametambulishwa rasmi akilamba kiasi cha Sh 180 milioni. Ndayiragije alionyesha uwezo wake na Mbao badae akaibukia KMC na sasa Azam imemtangaza jana kuwa kocha wao mpya wa kuchukua nafasi ya Mholanzi, Hans van Der Pluijm.

 

Kocha huyo Mrundi amesaini mkataba wa miaka miwili wa kutua Azam FC ambapo Spoti Xtra limejiongeza likaona mshahara wake ambapo atakuwa anakunja kiasi cha Sh milioni 7.5 kila mwezi mwezi.


Kutokana na kiasi hicho kwa muda wote wa miaka miwili kocha huyo raia wa Burundi atakunja kiasi cha milioni 180 lakini kwa masharti ya kubeba makombe. Akizungumza na Spoti Xtra, Ndayiragije amesema: “Azam FC
wameniamini, nina imani safari itakuwa nzuri.

 

Sitabadilisha kitu chochote ndani ya Azam, nitaendeleza na kuboresha zaidi, nitafanya kazi vile vyote ambavyo Azam wanavihitaji lakini kikubwa hasa ni hapa ndani ya ligi.”

 

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema: “Tulifanya tathmini kubwa sana kabla ya kumsajili.

 

Tuliangalia faili lake na tukajiridhisha kwamba yuko vizuri kutokana na rekodi zake.” “Anatakiwa kuhakikisha kila kombe lililopo mbele yetu analipa kipaumbele. Hatuchagui kombe kwanza ni kutetea ubingwa wa Kagame kisha Kombe la Shirikisho ambapo kwa msimu huu tunataka tukashindane na siyo kushiriki,”alisema Popat.

MUSA MATEJA NA SAID ALL

Comments are closed.