The House of Favourite Newspapers
gunners X

Ndege Yaangukia Gari Ikitua Kwa Dharura barabarani

0

Nchini Marekani, ndege ndogo imeanguka ghafla na kugonga gari kwenye barabara kuu ya I-95 huko Cocoa, Florida, siku ya Jumatatu saa 11 jioni kwa saa za huko, ikidaiwa kutua kwa dharura.

Tukio hilo lilitokea nyuma ya Toyota Camry ya mwaka 2023, huku ndege ikijaribu kutua kwa dharura. Video ya dashcam iliyopatikana kutoka kwa dereva aliyekuwa nyuma ya gari hilo, mwanamke mwenye miaka 57, ilionyesha ndege ikidondoka sekunde chache kabla ya kugonga gari. Dereva ameripotiwa kujeruhiwa kidogo tu, huku rubani mwenye miaka 27 na abiria wake wote wakipona bila madhara.

Mashuhuda walieleza kuona ndege ikidondoka kutoka angani na kurusha cheche, hali iliyosababisha uharibifu kwenye gari na sehemu ya mbele ya ndege kutenguka, kulingana na picha zilizopatikana eneo la tukio.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Marekani (FAA) imeanza uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha hitilafu iliyosababisha ndege hiyo kutua kwa dharura. Uchunguzi unaangazia usalama wa ndege na hatua zinazohitajika kuhakikisha tukio kama hili halitokei tena.

Leave A Reply